Home Makala Singida Bss Yakomaa na Morrison,Phiri

Singida Bss Yakomaa na Morrison,Phiri

by Sports Leo
0 comments

Tayari ikiwa na uhakika wa kushiriki katika michuano ya kimataifa msimu ujao klabu ya Singida Big Stars imeanza maandalizi ya msimu ujao kwa kukisuka kikosi cha timu hiyo kwa kuwasajili mastaa Moses Phiri na Benard Morrison.

Klabu hiyo mpaka sasa imeshafanya mazungumzo na Morrison huku wakionyesha kukubaliana baadhi ya mambo hasa baada ya timu yake ya Yanga sc kuonyesha nia ya kutoendelea nae ikidaiwa mpaka sasa hawajampa ofa ya mkataba mpya wa kusalia klabuni hapo.

“Ishu ya Morrison ilipofikia sidhani kama kunaweza kutokea mabadiliko yoyote ni kuhakikishie utamuona msimu ujao akiwa na timu yetu, ni mchezaji mkubwa ambaye tunaona anaweza kutusaidia,” kilisema chanzo cha ndani kutoka Singida Big Stars

banner

Katika mazungumzo ambayo bado hayajakamilika kizingiti pekee ni Azam Fc ambao nao inadaiwa kuwa wanamnyemelea staa huyu pamoja na Moses Phiri ambaye bado mazungumzo na mabosi wa Singida Big stars bado hayajafikia pazuri.

Phiri aliyesajiliwa na Simba sc akitokea Power dyanamos ya Zambia amewasilisha ombi la kuondoka klabuni hapo baada ya kocha Roberto Oliveira kutokua na imani nae kiasi cha kumuanzisha benchi mara kwa mara akishindwa kumpa hata dakika kumi.

Azam Fc nao wapo katika mbio za kuwawania mastaa hao huku wakijivunia zaidi kuwa na mazingira mazuri ya mastaa hao kuishi pamoja na mishahara minoni kwa mastaa hao.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited