Home Makala Staa Wa Ulaya Arejea Al Ahly

Staa Wa Ulaya Arejea Al Ahly

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Al-Ahly imethibitisha kuwa Mlinzi wao wa kushoto mwenye magoli 50 katika klabu hiyo Ali Maaloul aliyeukosa mchezo dhidi ya Simbaa sc jijini Dar es salaam amerejea kwenye kikosi hicho Kuelekea mechi ya marudiano ya AFL dhidi ya Simba huko Misri,

Pamoja na staa huyo pia klabu hiyo imethibitisha kuwa Emam Ashour nae atakuwa seheme ya Wachezaji watakaoitumikia klabu hiyo kwenye mchezo huo ujao wa AFL dhidi ya Simba sc utakaofanyika nchini humo.

Pia klabu hiyo imetangaza kwamba mshambuliaji wao mpya ambaye amewahi kucheza ligi kuu ya Ufaransa na Ujerumani Anthony Modeste ambaye hakuweza kusafiri na wenzake kwenda nao Dar es Salaam kwenye mchezo wa awali wa AFL dhidi ya Simba Kutokana na Masuala ya Kiafya kwa upande wake, nae amerejea kwenye kikosi Kuelekea mechi hiyo.

banner

Simba sc itakua na wakati mgumu kuwadhibiti waarabu hao katika mchezo wa marudiano nchini humo kutokana na ugumu wa timu hiyo hasa inapokua mbele ya mashabiki wake huku matokeo ya awali ya 2-2 yakiwapa nguvu wenyeji.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited