Home Makala Tshitshimbi Bado Kidogo

Tshitshimbi Bado Kidogo

by Sports Leo
0 comments

Taarifa kutoka kwa idala ya tiba ya klabu ya Yanga, inabainisha Nahodha Papy Tshishimbi huenda akakosa mechi za mwanzo ligi itakaporejea akiuguza jeraha la goti alilopata kwenye mazoezi ya timu hiyo

Mcongomani huyo leo atawashuhudia wenzake wakijipima dhidi KMC, mchezo wa kirafiki ambao utapigwa uwanja wa Uhuru

Daktari wa Yanga Dk Shecky Mngazija, amesema Tshishimbi alipata jeraha baada ya kuteguka mguu wake wa kulia

Amesema kiungo huyo bado yupo chini ya uangalizi wa daktari hadi pale hali ya jareha lake litakapopona.

“Kwa sasa Tshishimbi yupo chini ya uangalizi wa daktari kila siku anatakiwa kuhudhuria hospitalini kuangaliwa maendeleo yake,” alisema Mngazija

Cc:Youngsportsupdates

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited