Uongozi wa timu ya wananchi Yanga umekanusha kuwa hawakumtuhumu mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam ,Paul Makonda kuhusu jambo lolote linalohusiana na timu yao ya Yanga.
Taarifa hiyo ilisambaa kwenye mitando ya kijamii kuwa Yanga haikuwa na uwezo wa kuifunga Simba huku ikielezwa kuwa barua hiyo iliyosambazwa ilikuwa ni ya watu ambao si wa kutoka katika ofisi ya klabu hiyo.
Katibu mkuu wa Yanga ,David Ruhango amekataa taarifa hiyo iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na ameeleza kuwa yanga haihusiki kwa namna yoyote na taarifa hizo kuhusu tuhuma za klabu ya Yanga kwa mkuu wa mkoa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.