Home Makala Wameyakanyaga

Wameyakanyaga

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Tanzania Prisons Fc imekubali kipigo cha mabao 7-1 kutoka kwa Simba sc katika mchezo wa ligi kuu nchini ukiofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Wajelajela hao waliingia mchezo wakiwa na ahadi ya kupewa kiasi cha Shilingi milioni 30 endapo wangeshinda mchezo huo kutoka kwa wadhamini wao wa Silent Ocean lakini mpaka dakika tisini zinaisha hawakuamini kilichowatokea baada ya kukubali kipigo hicho kitakatifu kutoka kwa Mnyama.

Bao la mapema la John Boko dakika ya 12 ya mchezo lilisawazishwa Jeremiah Juma dakika ya 29 na kuwapa matumaini Prisons ya kuondoka na kitita hicho lakini walikutana na mvua ya mabao kutoka kwa Bocco aliyefunga mengine dakika za 46 na 62 huku Saido Ntibanzokiza aliyecheza mchezo wake wa kwanza klabuni hapo akifunga Hattrick dakika za 60,63 na 70 huku pia Shomari Kapombe nae alifunga bao la mwisho kwa Simba sc.

banner

Simba sc sasa imefikisha alama 44 nyuma ya Yanga sc iliyopo kileleni ikiwa na alama 47 huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi ikiwasubiri Mtibwa Sugar ili kukamilisha raundi ya 19 ya ligi kuu ambapo ligi itasimama kupisha michuano ya kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited