Home Makala Wanda Icard Amkolezea Mumewe Arsenal

Wanda Icard Amkolezea Mumewe Arsenal

by Sports Leo
0 comments

Mke wa mshambuliaji Mauro Icard wa Paris Saint -Germain (PSG) anayecheza huko kwa mkopo akitokea Inter Milan,Wanda Nara amechochea suala la mumewe  kusepa ndani ya timu hiyo na kuibukia Arsenal.

Wanda Nara ambaye ni wakala wa Icard na mke alisema hayo baada ya mtoto wao wa kiume kuvalishwa jezi ya timu ya Arsenal ambapo inaelezwa kuwa kitendo hicho wataalamu wa mambo wanatafsri kuwa ni dalili za mwanzo kabisa kuichochea Arsenal ifanye kweli na Mauro kuwa mbadala wa Pierre Emerick Aubameyang ambaye bado hajaongeza mkataba.

Mauro Icard ametupia jumla ya mabao 20 katika michezo 31 aliyocheza ndani ya PSG msimu huu na klabu hiyo imeshapokea ubingwa wa ligi kuu ufaransa baada ya ligi hiyo kufutwa kutokana na janga la Corona.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited