Home Makala Wawili Kutemwa Azam Fc

Wawili Kutemwa Azam Fc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam ina mpango wa kuachana na wachezaji wale wawili kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi January ili kupisha usajili wa beki wa zamani wa Yanga Djuma Shaban na Mlinda lango wa Tabora United raia wa Nigeria John Noble.
Mabosi wa klabu hiyo mpaka sasa hawajaamua rasmi nani na nani watawapisha mastaa hao wapya lakini iko wazi katika ya makipa Ali Ahmada na Abdulai Idrissu mmoja atampisha Noble kikosini humo kutokana na ukweli ni ngumu kuwa na makipa watatu wa kigeni.

Taarifa zinadai kuwa tayari wachezaji hao wameshakubalina na Azam Fc kuhusu maslahi binafsi huku Noble akisajiliwa na Azam atakuwa analipwa zaidi ya Million 21 mara tatu zaidi ya mshahara anaolipwa Tabora United, kwasasa analipwa Million 7.
Djuma Shabani yeye tayari ameshaanza mazoezi na kikosi cha Azam Fc ili kujiweka fiti hasa baada ya kumalizana na Yanga sc akiungana na mwenzake Yannick Bangala ambaye yeye usajili wake ulikamilika mapema.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited