Home Makala Wawili Waingia Anga Za Yanga

Wawili Waingia Anga Za Yanga

by Sports Leo
0 comments

Baada ya Yanga kuachana na Luc Eymael ambaye alikuwa kocha mkuu wa timu hiyo wanawapigia hesabu za kasi makocha wenye uzoefu na Ligi kuu bara ambao ni Patrick Aussems kutoka Simba Sc na Hitimana Thiery wa Namungo Fc.

Yanga Sc imeanza mchakato wa kumleta kocha mpya ambaye atafanya kazi ya kukinoa kikosi kwa ajili ya msimu ujao na miongoni mwa majina yaliyopendekezwa ni pamoja na Aussems na Thiery.

Simon Patrick ambaye ni kaimu katibu wa Yanga ,amesema kuwa kwa sasa wanaendelea na mchakato wa kumtafuta kocha mambo yakiwa sawa wataweka wazi,japo ni kweli Thiery amekuwa bora kwani amemaliza ligi akiwa ndani ya tano bora na aliweza kuwasumbua Yanga hata Simba walipokutana ndani ya uwanja.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited