Ratiba ya awali ya michuano ya klabu bingwa Afrika imetoka ambapo wawakilishi wa Tanzania timu za Simba na Yanga zimepangwa kuanza na timu za Township Rollers ya Botswana na Ud Songo ya Msumbiji.
Katika ratiba hiyo iliyotoka jana inaonesha kuwa mechi za awali zitapigwa kati ya agosti 9-11 na za marudiano zitakua kati ya Agosti 23-25 huku Yanga ikianzia nyumbani dhidi ya Wabotswana hao ambao ilivaana nao jijini Dar es salaam mwaka 2018 na kufungwa kwa mabao 2-1 likiwemo bao la kideoni ambapo zilipigwa pasi zaidi ya kumi kabla ya goli hilo kupatikana na mshindi wa mechi hizo atakutana na mshindi kati ya Green Mamba na Zesco united.
Simba sc iliyoweka kambi nchini Afrika Kusini itaanzia mechi ugenini kati ya tarehe hizo na kisha kurudiana nyumbani ambapo mshindi ataavana na mshindi kati ya Big Bullets ya Malawi na Fc Platnum ya Zimbabwe mechi zikichezwa kati ya Septemba 13-15 na marudiano ikiwa ni Septemba 27-29.
Baada ya kucheza mechi hizo za awali na endapo timu hizo zikifanikiwa kufuzu basi moja kwa moja zitakua zimefanikiwa kuingia hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika.
Kwa upande wa kombe la shirikisho ambako wawakilishi wa Tanzania ni Azam fc na Kmc ya kinondoni inayoshiriki michuano ya kimataifa kwa mara ya kwanza ratiba inaonyesha kuwa matajiri wa chamazi watavaana na Fasil Kenema ya Ethiopia katika ya Agosti 9-11 ugenini na marudio yatafanyika nchini tarehe 23-25.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mshindi wa mechi hiyo atavaana na mshindi kati ya Triangle ya Zimbabwe na Rukinzo ya Burundi na atakayeshinda atakua amefuzu kwenda hatua ya makundi.
Kwa upande wa Kmc yenyewe itawakaribisha timu ya As Kigali anayoichezea kiungo aliyetemwa na Simba sc Haruna Niyonzima na mshindi wa mechi hiyo atavaana na mshindi kati ya Proline ya Uganda na Master Security ya Malawi.
Hata hivyo ratiba hiyo imeweka wingu zito kuhusu maadhimisho ya sherehe za Simba day ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 8 Agosti na ikizingatiwa Simba itaanzia ugenini hivyo tarehe hiyo inawezekana timu ikawa imesafiri ama itakua inajiandaa na mechi hiyo hivyo kucheza mechi siku ya Simba day inakuwa ni ngumu kwa kuzingatia afya ya wachezaji huku kwa upande wa Yanga ikiwa siku ya kilele cha wiki hiyo ni Agosti 4 na itakua na mechi dhidi ya As Vita sasa inategemea na ratiba husiki ya timu hiyo baada ya kupata ratiba ya ligi ya mabingwa.