Home Makala Yanga sc Inogile,Yazidi Kukaa Kileleni

Yanga sc Inogile,Yazidi Kukaa Kileleni

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imezidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini baada ya kuifunga klabu ya Polisi Tanzania kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Katika mchezo huo mkali na wa kusisimua Yanga sc ilikosa huduma ya kiungo mshambuliaji Feisal Salum kutokana na majeraha huku nafasi yake ikichukuliwa na Farid  Musa ambaye alikua na mchezo mzuri hasa eneo la kati huku akikosa ubunifu wa kufikisha mipira kwa Fiston Mayele hali iliyosababisha mpaka mapumziko timu zote kwenda zikiwa hazijafungana.

Kipindi cha pili Yanga sc walifanya mabadiliko kwa kumuingiza Dickson Ambundo kuchukua nafasi ya Farid Musa hali iliyoleta uchangamfu hasa eneo la kiungo na kumfanya Fiston Mayele kupata huduma nzuri huku pasi ya pembeni ya Ambundo ikimfikia Mayele aliyewatoka mabeki wa Polisi Tanzania na kutoa pasi kwa Ambundo aliyefunga kiulaini dakika ya 63 ya mchezo bao ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.

banner

Yanga sc kwa ushindi huo imefikisha alama 35 ikiwa juu ya msimamo wa ligi kuu huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Simba sc ikiwa na alama 25 ikiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Kagera Sugar.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited