Home Makala Yanga Sc Kurejea Dar August 2.

Yanga Sc Kurejea Dar August 2.

by Dennis Msotwa
0 comments

Baada ya maandalizi ya wiki tatu mkoani Morogoro, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam Ijumaa August 02 2019 siku mbili kabla ya siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi

Yanga itakuwa tayari kwa tukio hilo la kihistoria litakalofanyika Jumapili ya August 04, uwanja wa Taifa

Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Mwinyi Zahera aliyewasili mkoani Morogoro jana, atakuwa na takribani siku tano kukinoa kikosi chake kabla ya kuivaa Kariobangi Sharks Jumapili

Mcongomani huyo amesema amefurahishwa na maandalizi yaliyofanywa kocha Msaidizi Noel Mwandila wakati ambao yeye hakuwepo

Amesema atatumia muda uliobaki kuwaandaa wachezaji wake kimbinu tayari kwa mchezo wa Jumapili na mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers

Yanga ikiwa chini ya Noel Mwandila, imecheza michezo mitano ya kirafiki na kufanikiwa kushinda yote huku ikifunga mabao zaidi ya ishirini na kufungwa mabao yasiyozidi matatu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited