Home Makala Yanga Sc Yaidunga Prisons 5-0

Yanga Sc Yaidunga Prisons 5-0

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuchukua alama tatu katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini dhidi ya Klabu ya Tanzania Prisons baada ya kuifunga kwa mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Yanga sc ikiingia uwanjani bila mshambuliaji wake Stephan Aziz Ki ambaye ameuzwa nchini Morocco ilianza kwa kasi ikiwategemea Clement Mzize na Pacome Zouzoua sambamba na Prince Dube ambapo mashabiki walilazimika kusubiri mpaka dakika ya 31 ambapo krosi ya Israel Mwenda ilimkuta Mudathir Yahaya aliyefunga kwa kichwa na kufungua kalamu ya mabao.

banner

Clement Mzize alipokea pasi safi ya Mudathir Yahaya na kumpiga chenga kipa Sebusebu Samson na kumpasia mpira Chama aliyefunga bao la pili kwa Yanga sc dakika ya 35 ya mchezo.

Mudathir bado aliendelea kuwa tishio kwa Prisons baada ya kumpa presha beki Jumanne Elifadhil na kumpora mpira na kumpasia Pacome aliyefunga bao la tatu kwa Yanga sc dakika ya 56 huku pia dakika tano baadae Shadrack Boka alitoa pasi ya juu kwa Israel Mwenda aliyefunga bao la nne kwa Yanga sc kwa kichwa.

Pacome Zouzoua alifunga bao tano kwa Yanga sc kutokana na uzembe wa walinzi wa Prisons kuondoka mpira golini na kumkuta mfungaji dakika ya 71 ya mchezo huo.

Dakika 90 zilimalizika kwa Yanga SC kupata alama tatu na kufikisha alama 74 kileleni mwa msimamo huku Tanzania Prisons wakisalia nafasi ya 13 na alama 30 katika michezo 29 ya ligi kuu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited