Klabu ya Yanga sc imeendelea na msimamo wake wa kuhitaji fedha zake za ubingwa wa Kombe la shirikisho la Crdb nchini kwa misimu mitatu mfululizo licha ya kuitwa na shirikisho la soka nchini (TFF) kwa ajili ya kikao.
Mapema hivi leo mtendaji mkuu wa klabu hiyo Andre Mtine alifika katika ofisi za Shirikisho hilo akiwa na nyaraka mbalimbali pamoja na barua akiomba klabu hiyo kupatiwa fedha zake kisha kuondoka licha ya kuitwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Wilfred Kidao.
Punde tu baada ya kutoka mtendaji huyo alinukuriwa akisema kuwa wao hawahitaji kikao bali kinachohitajika ni fedha pekee kwa sasa.
“Yanga tunachohitaji ni hela zetu za ubingwa, Tarehe 28 inabidi tusafiri kwenda Zanzibar kuna gharama za usafiri, bonus na mengine tutalipaje?. Duniani hakuna nchi ambayo bingwa hapewi hela yake”.Alisema mtine kwa lugha ya kiingereza.
“Naomba niulize ni wapi meona wametaja Kiasi anachopaswa kulipwa bingwa wa kombe la Shirikisho, ni wapi? Wanaficha taarifa” .Alimalizia Andre Mtine ambaye ni raia wa Zambia.
Yanga sc imeendelea na msimamo wake wa kutocheza mchezo wa derby ya Kariakoo dhidi ya Simba Sc ambapo kwa sasa pia wanampango wa kugomea mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho la Crdb nchini dhidi ya Singida Black Stars Juni 28 mwaka huu.