Klabu ya Yanga Sc imekamilisha usajili wa winga wa Tabora United Offen Chikola kuelekea msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya Kimataifa 2024-2025.
Baada ya majadiliano ya pande mbili Yanga Sc wamemalizia vitu kadhaa na Tabora United Fc ambapo tayari Offen Chikola amesaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo.
Kiwango bora alichoonyesha msimu huu uliomalizika kimewafanya mabosi wa yanga kukaa chini na kumaliza dili la winga huyo mapema wakiwawahi Simba Sc na Azam Fc ambao walikua wanamvizia.
Kiungo huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi za winga wa kulia na kushoto pamoja na nafasi zote za ushambuliaji msimu huu alifunga mabao saba na kutoa pasi saba za mabao katika klabu hiyo.