Home Soka Yanga Sc Yapandisha Kombe Mlima K’njaro

Yanga Sc Yapandisha Kombe Mlima K’njaro

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imeamua kulipeleka kombe lake la ligi kuu iliyolitwaa msimu huu katika kilele cha mlima Kilimanjaro ikiwa ni ishara ya kuonyesha mafanikio yake msimu huu baada ya kutwaa taji la hilo kwa mara ya tatu mfululizo na mara ya 30 kwa ujumla wake.

Yanga sc ilitwaa taji hilo la 30 katika historia ya klabu hiyo baada ya kumaliza ligi kuu ikiwa na alama 80 baada ya kucheza jumla ya michezo 30 ya ligi kuu ya soka ya Nbc Tanzania Bara.

Baada ya kukabidhiwa kombe hilo na wadhamini wakuu wa ligi kuu benki ya Nbc katika uwanja wa Benjamini Mkapa baada ya mchezo dhidi ya Tabora United ambapo timu hiyo ilishinda kwa mabao 4-0 na kufanya shangwe kubwa huku kesho yake Jumapili Mei 26 wakifanya paredi kubwa mpaka katika uwanja wa Kaunda yalipo makao makuu ya klabu hiyo.

banner

Baada ya shamra hizo sasa ni zamu ya mashabiki kuliona taji hilo likiwa kileleni mwa mlima huo mrefu barani Afrika na wa pili duniani ambapo tayari safari ya kukitafuta kilele hicho imeshaanza.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited