Klabu ya soka ya Yanga sc imetangaza viingilio vy amchezo wake wa kwanza wa hatua ya awali katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Asas Fc ya nchini Djibout utakaofanyika siku ya Jumapili August 20 katika uwanja wa Chamazi Complex.
Akizungmza na waandishi wa habari mkuu wa Idara ya Habari ya klabu hiyo Ally Kamwe alisema kuwa kutokana na mipango ya uongozi kiingilio cha juu kitakua kiasi cha shilingi elfu thelasini na kiingilio cha chini kitakua ni elfu tano tu katika eneo la mzunguko.
“Napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha Wanahabari na Mashabiki wetu wote wanaotufatilia Mubashara kupitia Azam TV na leo nimekuja kuwapa taarifa za Mashindano ya Kimataifa na Hali ya Kikosi chetu baada ya mechi ya fainali Ngao Jamii,