Klabu ya Yanga sc imempokea Mshambuliaji David Moringa (Falcao) raia wa Kongo kuja kusaini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo jana usiku katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa J.K Nyerere.
Mshambuliaji huyo mwenye mwili mkakamavu aliwasili uwanjani hapo na kupokelewa na Afisa Habari msaidizi wa klabu hiyo Godlisten Anderson(Chicharito) na kuelekea moja kwa moja hotelini.
Inadaiwa mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu za Fc Lupopo atasaini mkataba wa miaka miwili na atajiunga na kikosi kilichopo kambini Morogoro hii leo.