Home Soka Aston Villa Waichapa Arsenal

Aston Villa Waichapa Arsenal

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Aston Villa ya Uingereza anayoichezea mtanzania Mbwana Samatta imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Arsenal na kufufua matumaini ya kutoshuka daraja nchini humo.

Bao hilo la dakika ya 27 lililofungwa na Mohamed Trezeguet aliyesajili majira ya joto kwa dau la paundi milioni 8.5 limeifanya Villa kupanda mpaka nafasi ya 17 katika msimamo huk wakihitaji ushindi katika mchezo unaofuata dhidi ya Westham siku ya jumapili huku wakiombea Watford afungwe na Arsenal.

“Tulikua na matarajio makubwa zaidi ya kumaliza nafasi ya 17 mwanzoni mwa msimu lakini tuna furaha kutulia hapo sasa” Alisema Smith kocha wa Aston Villa.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited