Home Soka Athur Melo Atua Juve

Athur Melo Atua Juve

by Sports Leo
0 comments

Arthur Melo amesaini kandarasi ya miaka 5 Juventus hadi 2025 akitokea klabu ya Barcelona baada ya klabu hizo kuamua kubadilishana na Miralem Pjanic akielekea upande wa Barcelona.

Kiungo huyo amekamilisha dili hilo ambapo  tayari kashapimwa afya huku  upande wa Miralem Pjanic huko ukiwa katika hatua za mwisho kukamilika huko Barca.

Kinda huyo licha ya kukamilisha usajili huo ataendelea kusalia Barca akishiriki michuano ya La liga na Uefa mpaka mwishoni mwa msimu ndio atajiunga na vibibi kizee cha Turin ambapo alikamilisha vipimo vya afya siku ya Jumapili alipopaa kuelekea Turin baada ya mchezo dhidi ya Certa Vigo alioingia kipindi cha pili.

banner

Inadaiwa uhamisho huo umeigharimu Juve kiasi cha paundi 72milioni huku ule wa Pjanic ukiwa na thamani ya paundi 60 milioni.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited