Home Soka Azam Fc Yasajili Kifaa

Azam Fc Yasajili Kifaa

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc imekamilisha usajili wa mchezaji Franck Tiesse raia wa Ivory Coast, kutoka Stade Malien ya Mali kwa mkataba wa miaka miwili kuanzia msimu ujao wa 2024/25.

Frank ni kiungo mshambuliaji mwenye uwezo wa kucheza nafasi zote za eneo hilo ikiwemo kutokea pembeni mwa uwanja ambapo amejiunga na Azam Fc baada ya kukamilisha vipimo vya afya katika Hospitali ya Aghakan jijini Dar es salaam.

banner

Mpaka sasa kikosi cha Azam Fc kina mawinga kama Idd Selemani Nado,Kipre Junior,Gibril Sillah,Ayoub Lyanga pamoja na wengine hivyo staa huyo hana budi kukaza buti ili kupata nafasi kikosini humo kwani waliopo wapo vizuri.

Azam Fc msimu ujao ina uhakika wa kushiriki michuano ya kimataifa hivyo wameamua kuanza mapema maboresho ya kikosi cha ili kujiandaa na michuano hiyo ikiwa ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Azam, ikiwa tayari Aprili 19,2024 ilimtangaza Yoro Mamadou Diaby raia wa Mali akitokea kwenye akademi ya Yaleen Olympique.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited