Home Soka Azam yawafuata Kanema Alfajiri

Azam yawafuata Kanema Alfajiri

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Azam Fc leo jumatano imesafiri kwenda nchini Ethiopia kuwafata timu ya Fasil Kenama katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika raundi ya kwanza utakaopigwa nchini humo msiku ya jumamosi.

Msafara wa Azam FC umeondoka na wachezaji 23, watu watano wa benchi la ufundi wakiongozwa na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije pamoja na viongozi na maofisa wa timu hiyo.

banner

Aidha katika kukabiliana na changamoto za ugenini, Azam FC ilitanguliza sehemu ya uongozi wake tokea juzi wakiongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’, ili kuandaa mambo mbalimbali na taratibu zote za timu ikiwa huko.

Azam inabidi kutafuta matokeo ya ushindi ugenini ili kujiwekea mazingira ya kufuzu katika mchezo wa pili utakaofanyika nchini Tanzania.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited