Saa saba ya maajabu msimbazi imewadia kwa timu hiyo kumpa mkataba wa miaka miwili Beki wa Kimataifa kutoka Brazil Gerson Fraga Vieira mwenye miaka 26 akitokea katika Timu ATK ya ligi kuu nchini India.
Fraga mwenye uso na mwili wa kitanashati amesaini mkataba huo mbele kiongozi wa Simba Zacharia Hanspope ili kujiunga na mabingwa hao mara mbili mfululizo wa ligi kuu Tanzania bara na washiriki ya ligi ya mabingwa mpaka hatua ya nane bora walipotolewa na Tp Mazembe ya Kongo.

Kikosi cha vijana cha timu ya Taifa ya Brazil ambacho kina mastaa kama neymar,coutinho,allison na Casemiro.Mwenye duara ndio mchezaji aliyesajiliwa na Simba sc Gerson Fraga Vieira.
Beki huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo mkabaji aliwahi kuwa nahodha wa kikosi cha vijana cha Brazil kilichokua na mastaa kama Neymar wa Psg,Philipe Coutinho wa Barcelona,Kipa anayeidakia Liverpool ya Uingereza Allison na Wengine kibao.Pia alikuwamo katika kikosi cha Taifa hilo chini ya miaka 20 kilichoshiriki michuano mbalimbali.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.