Fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) yaliyotakiwa kufanyika mwaka huu nchini Cameroon yamesogezwa mbele na sasa ni rasmi yatafanyika mwaka 2021 mwezi januari.
Tanzania ni kati ya timu zilizofuzu michuano hii baada ya kumtoa jirani yake Kenya pamoja na Sudan huku Uganda na Rwanda nazo zimefuzu kwa upande wa timu kutoka Afrika Mashariki.
Hii ni mara ya pili kwa Caf kughairisha michuano hiyo ambapo ilihamishwa kutoka nchini Ethiopia kwenda Cameroon na ilipangwa kuanza mapema mwaka huu ambapo pia ilighairishwa mpaka April 25 ambapo sasa imehamishiwa January mwakani.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.