Baada ya Klabu ya Yanga kutangaza kuanza mchakato wa kutaka kumrejesha mshambuliaji wa kimataifa wa DR Congo, Heritier Makambo anayecheza Horoya AC ya Guinea,Afisa habari wa Klabu hiyo Elhadj Ibrahima Kalil amesema hamna ofa wala mawasiliano yoyote kutoka Yanga ya kumtaka Makambo.
-brahima amedai kuwa bado wana mkataba mrefu na mshambuliaji huyo. Pia amesema Makambo ni mchezaji muhimu kwenye kikosi chao lakini kama Yanga wapo tayari waandae dau la dola 130,000 (zaidi ya Milioni 300 za kitanzania) kuvunja mkataba wa miaka miwili uliobaki.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.