Home Soka David Luiz Njia Panda

David Luiz Njia Panda

by Sports Leo
0 comments

Kufuatia kipigo cha mabao 3-0 ilichokutana nacho Arsena hapo jana kutoka kwa klabu ya Manchester City katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza umeweka rehani hatma ya beki huyo katika klabu yake.

Luiz aliyewahi kuichezea Psg na Chelsea kwa wakati mbalimbali aliingia katika mchezo huo kipindi cha pili ambapo alionyesha kiwango kibaya ikiwemo kusababisha penati pamoja na kuonyeshwa kadi nyekundu.

“Sijui nini kitatokea kwenye mkataba wake. Najua nini kilichotokea leo (Jana) Kulikuwa na sababu kwanini sikumuanzisha mwanzo (mchezo dhidi ya City)” Alijibu Kocha Mikel Arteta alipoulizwa kuhusu mkataba wa beki huyo.

banner

David Luiz naye alisema”Ningetakiwa kuchukua uamuzi tofauti katika miezi miwili iliyopita. Kujaribu na kuamua hatma yangu, kujaribu na kuamua mapema iwezekanavyo. Haikuwa kosa la timu, lilikuwa kosa langu. Kocha ni mzuri” .

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited