27
Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) imelichagua Goli la kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Simba,Luis Miquissone kama goli bora la Wiki la Ligi ya Mabingwa Afrika.
Goli hilo la Luis Miquissone alilifunga katika mechi dhidi ya miamba ya soka barani Africa Al Ahly kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Februari 23.
Goli hilo pekee liliwapa ushindi mabingwa hao Vodacom Premier league na kufanikiwa kuongoza kundi A wakiwa na jumla ya alama 6.