Home Soka Ihefu Fc Yabadili Jina

Ihefu Fc Yabadili Jina

by Sports Leo
0 comments

Uongozi wa klabu ya  Ihefu FC ambao siku za karibuni umeyahamisha makazi ya klabu hiyo kutoka Mbarali Mbeya na kwenda mkoani Singida, na hivyo kufanya mabadiliko ya jina la timu na sasa kutambulika kama Singida Black Stars Sports Club.

Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kwenda kwa umma  imesema kwamba  lengo la kubadilisha jina la timu hiyo  ni kuiunganisha na wananchi wa mkoa wa Singida ambako sasa timu hiyo itakua inapatikana na itatumia uwanja wa CCM Liti kama uwanja wake wa nyumbani.

Katika taarifa hiyo pia klabu hiyo imeeleza kuwa taratibu zote za usajili wa jina hilo tayari zimekamilika kwa kufuata miongozo, kanuni na taratibu zote za Nchi, Baraza la Michezo (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

banner

Awali ilianza kwa klabu ya Singida Big Stars kubadilisha jina na kuwa Singida Fountaine Gate Fc kisha baadae mastaa wake muhimu wakaondoka klabuni hapo na kuhamia Ihefu Fc ambapo baadae Ihefu ilihamia mkoani Singida na Singida FG yenyewe iliamua kuhamia mkoani Mwanza ilipo mpaka sasa.

Pamoja na kufanya mabadiliko hayo bado mashabiki wa soka nchini wamekua na mvutano wa maoni kuhusu uamuzi huo huku wengine wakiona ni sahihi na wengine wakiona hatua hiyo ni moja ya kusigina maendeleo ya soka nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited