17
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya Yanga sc Injinia Hersi Said ametua Africa kusini akitokea DR Congo kuangalia uwezekano wa kukamilisha usajili Lazaraus Kambole kutoka klabu ya Kaizer Chief.
Habari za ndani zinaeleza kuwa bosi huyo wa GSMÂ alishafanya mazungumzo ya awali na uongozi wa Kaizer chief walipokuja kucheza na Simba sc katika mechi ya robo fainali ya Caf champion League mkondo wa pili ambapo
Amakhos walikubali kipigo cha goli 3-0 kutoka kwa Simba sc.
Kama Hersi Said atafikia makubaliano na uongozi wa Kaizer chief basi Kuna uwezekano mkubwa wa Kambole kutua Jangwani kwani mshambuliaji huyo raia wa Zambia amekosa nafasi katika kikosi cha Amakhos na tayari anatajwa kuwa katika orodha ya wachezaji ambao wataachwa baada ya mkataba wake kuisha.