Home Soka Jezi Ya Morrison Yawa Lulu

Jezi Ya Morrison Yawa Lulu

by Sports Leo
0 comments

Jezi ya kiungo wa Yanga Benard Morrison imeonekana kuwa lulu baada ya mashabiki kuigombania kama njugu hasa wakati wa mchezo baina ya watani wa jadi Yanga na Simba.

Kwa mujibu wa Afisa Mhamasishaji wa klabu hiyo Antonio Nugaz jezi 1500 za Morrison ziliuzwa wakati wa kuelekea kwenye pambano la watani wa jadi.

“Awali tuliandaa jezi 1000 wakaja watu wakaomba tutengeneze nyingine za Morrison tukatengeneza 500 ambazo zote ziliisha”.

banner

Pia Nugaz alithibitisha kuwa baada ya Morrison,Jezi zilizonunuliwa zaidi ni za nahodha wa klabu hiyo Papy Kabamba Tshitshimbi ambaye alicheza mpira wa maana siku ya pambano la watani ambapo Yanga walishinda 1-0.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited