Home Soka Jezi Yanga Yazidi Kuchafuka

Jezi Yanga Yazidi Kuchafuka

by Dennis Msotwa
0 comments

Ni mwaka wa neema jangwani ndi unavyoweza kusema kwa sasa baada ya timu hiyo kupokea dili nono la udhamini kutoka kampuni ya GSM kupitia magodoro ya Gsm foam ambao wameingia mkataba wa mwaka mmoja kuidhamini klabu hiyo.

Haya yamekuja siku chache baada ya timu hiyo kupata udhamini mwingine kutoka kampuni ya gesi inayomilikiwa na bilionea Rostam Aziz kupitia bidhaa ya Taifa Gas ambao wanakaa mikononi mwa jezi za timu hiyo.

Udhamini huo wa Gsm unabaki kuwa siri kwa upande wa maslahi kama ilivyo mikataba mingine ambayo timu hiyo imeingia hivi karibuni.

banner

Hivi sasa Yanga ina udhamini wa makampuni kadhaa makubwa ikiwemo Sportpesa ambao ni wadhamini wakuu wanaokaa kifuani huku kampuni ya maji ya Watercom kupitia maji ya afya wakidhamini kama kinywaji kikuu cha kampuni hiyo wakati wa mechi na mazoezi na Taifa gas ambao hukaa mkononi huku Gsm foam watakaa mgongoni juu ya namba ya jezi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited