Wakala wa mshambuliaji wa Simba sc Meddie Kagere amethibitisha kumtafutia timu mshambuliaji huyo nchini Marekani ambapo anaweza kujiunga na timu hiyo msimu ujao endapo atafakisha mabao 25 ya ligi kuu na michuano mengine ambayo Simba sc inashiriki.
Wakala huyo Patrick Gakumba amesema tayari mchezaji tayari ana ofa kutoka Dallas Fc inayoshiriki ligi kuu nchini Marekani maarufu kama Major Soccer League ambapo moja ya masharti aliyopewa na timu hiyo ni kuhakikisha anafunga idadi hiyo ya magoli kwa msimu huu.
Kagere alijiunga na Simba sc akitokea Gormahia ya nchini Kenya ambapo toka ajiunge na timu hiyo amekua akifanya vizuri kiasi cha kuchukua tuzo mbalimbali ikiwemo ufungaji bora wa ligi kuu msimu uliopita.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.