Wakati mazoezi ya kikosi cha Simba kujiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya AS Vita yakizidi kupamba moto, wachezaji wawili wa mabingwa hao wa Tanzania, Luis Miquissone na Meddie Kagere ndio wanaochelewesha mipango ya miamba hiyo ya soka nchini, imeelezwa.
Katika mechi hiyo, Simba itakuwa ikihitaji sare tu ili kufuzu hatua ya robo fainali, wakati AS Vita yenyewe ikihitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi ya kufuzu hatua hiyo, wakati huu Al Ahly ambao watakuwa ugenini dhidi ya vibonde wa kundi hilo, Al-Merrikh ya Sudan yenye alama moja, nayo ikihitaji ushindi huku ikiombea Wekundu wa Msimbazi hao washinde ili nao wakate tiketi kabla ya mchezo wa mwisho.
Naye Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, alisema wachezaji wote waliokuwa na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wameungana na wenzao huku baadhi yao walikuwapo katika mataifa yao wakitarajiwa kuungana na wenzao jana isipokuwa Miquissone na Kagere.
Alisema Miquissone na Kagere wao wataripoti kambini leo Alhamisi kwa sababu timu zao za taifa zilikuwa na mechi juz juma nne
@sokaonline