Home Soka Kamusoko Amuweka Matatani Zahera

Kamusoko Amuweka Matatani Zahera

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mtaalamu wa staili ya kampa kampa tena Thabani skala Kamusoko amuweka matatani kocha wa Timu ya Yanga Mwinyi Zahera kufuatia kuwemo katika orodha ya wachezaji watakaopewa mkono wa kwaheri na klabu hiyo msimu huu.

Kiungo huyo wa zamani wa Njube sundowns na Dyanamos za Zimbabwe amemuweka matatani Zahera kufuatia kupandisha kiwango chake katika mechi za mwishoni mwa msimu wa ligi kuu kiasi cha kuitwa timu ya taifa ya Zimbabwe inayojiandaa na michuano ya Afcon nchini Misri huku kiwango chake katika mechi za awali za kupasha misuli kujiandaa na michuano hiyo akionyesha kiwango cha hali ya juu hususani mechi aliyocheza na Tanzania(Taifa stars).

Inadaiwa kufuatia Kiwango,Uzoefu na Nidhamu ya mchezaji huyo imewegawa baadhi ya vigogo wa jamgwani ambao baadhi wakikubaliana na ripoti ya Zahera kumtema huku wengine wakipinga na kutaka mkongwe huyo kubakishwa klabuni hapo kwani uzoefu wake ni muhimu.

banner

Kamusoko alisajiliwa na Yanga kutokea Fc Platinum ya Zimbabwe Mwaka 2015 na tangu asajiliwe alionyesha kiwango cha hali ya juu akiwa chini ya kocha Hans Van Plujm na msimu ulioisha alisumbuliwa na majeruhi yaliyosababisha kiwango chake kushuka.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited