Home Soka Kiingereza Chamnyima Dili Zahera

Kiingereza Chamnyima Dili Zahera

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa zamani wa Klabu ya Yanga Mkongo Mwiny Zahera amekataa kazi ya kuifundisha klabu ya Township Roller ya nchini Botswana baada ya kutofahamu kuzungumza lugha za kiingereza.

Zahera ambaye anayeishi nchini huku akienda Ufaransa na Kongo mara chache kuangalia familia na biashara anazungumza kwa usahihi lugha za kifaransa na kiswahili wakati akiwa hajui kiingereza ambacho ndio kinatumika sana nchini Botswana hivyo kushindwa kukubali dili hilo.

“Nimepigiwa simu na wakala kutoka Botswana akinieleza kwamba Klabu hiyo inatafuta kocha nakusema kwamba, vile nalikwenda kule na Yanga sc ndio wale viongozi wawo walinanii.. waliniomba nasikiya” Ameendelea Zahera.

banner

“Tukasumiliana naye nikamueleza kwamba Boo, mi siwezi kunanii… Kuenda kule ku Botswana sababu sijuwe kuzungumza nanii … Kingereza kwa hiyo itakuwa shida kwangu kuenda kule” Alisisitiza Zahera

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited