Kocha wa zamani wa klabu ya Simba sc Masoud Djuma amewapa tano klabu ya Yanga baada ya kusikia wanaisaka saini ya kiungo wa Rwanda Ally Niyonzima.
Kocha huyo ambaye amewahi kumnoa kiungo huyo wakati akiifundisha klabu ya As Kigali mwaka 2018 alisema kama Yanga watakamilisha dili hilo watakua wamelamba dume kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi tatu uwanjani.
Kwa mujibu wa kocha huyo mwenye mizuka awapo uwanjani Niyonzima ana uwezo wa kucheza kama beki wa kati pamoja na kiungo mkabaji au mshambuliaji.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.