Home Soka Kwa Molinga,Makambo Anasubiri

Kwa Molinga,Makambo Anasubiri

by Dennis Msotwa
0 comments

Kocha wa timu ya Yanga Mwinyi Zahera amesema mshambuliaji mpya wa timu hiyo David Molinga ni hatari kushinda Herritier Makambo aliyeichezea timu hiyo msimu uliopita.

Zahera amesema hayo jana wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya timu hiyo kumaliza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa kimataifa dhidi ya Zesco ambao utafanyika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

“Molinga ni mchezaji mzuri ndo mana ligi ya kongo alifunga mabao 15 wakati Makambo alifunga saba,Nina imani msimu huu atafunga magoli 15 au 20 na asipofanya hivyo nitatoa dola 1000”.

banner

Molinga alikua na wakati mgumu aliposajiliwa klabuni hapo baada ya kukosa nafasi za wazi za magoli hali iliyosababisha mashabiki kuanza kuponda kiwango chake japo siku za karibuni amefanikiwa kufunga mabao matatu katika mechi mbili za kirafiki alizocheza.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited