Home Soka Mashujaa Fc Yaikomalia Azam Chamazi

Mashujaa Fc Yaikomalia Azam Chamazi

by Sports Leo
0 comments

Kikosi cha timu ya Mashujaa Fc kimefanikiwa kuchukua alama moja katika mchezo uliomalizika kwa 0-0 dhidi ya Azam Fc katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es salaam baada ya kuzui kwa dakika zote 90 za mchezo huo.

Mashujaa Fc inayonolewa na Kocha Mohamed Barresi iliingia kwa heshima kubwa katika mchezo huo ikikaa nyuma ya mpira na kuwaacha Azam Fc kutawala dakika zote 90 za mchezo huo huku goli pekee ndio likikosekana licha ya Azam Fc kuanzisha mastaa wake wote wakiongozwa na Feisal Salum,Kipre Junior,Abdul Sopu na wengine.

Mashujaa Fc iliyoanza na mshambuliaji mmoja Reliants Lusajo nusra ipate bao kutokana na kukosa nafasi chache ilizotengeneza kwa kukosa umakini kidogo ambapo kipa Mohamed Mustafa alikua imara kuokoa hatari hizo.

banner

Azam Fc wamezidi kujiwekea mazingira magumu ya kumaliza katika nafasi mbili za juu kutokana na kushindwa kuongeza pengo la alama kati yake na Simba sc ambapo mpaka sasa Azam Fc ana alama 51 katika michezo 23 huku Simba sc ikiwa na alama 46 katika michezo 20 ya ligi kuu ya Nbc.

Endapo Simba Sc itafanikiwa kushinda michezo yake yote ya viporo itafikisha alama 55 na kuwaacha Azam Fc katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 51 ambapo watakua wanaweka rehani nafasi yao ya kushiriki michuano ya kimataifa endapo bingwa wa kombe la shirikisho atatoka nje ya timu nne za juu za ligi kuu nchini huku wao wakiendelea kupoteza alama.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited