Home Soka Mastaa Azam Fc Kuikosa Simba sc

Mastaa Azam Fc Kuikosa Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Mastaa wawili wa klabu ya Azam Fc Yahya Zaidi na Kiungo Ally Niyonzima wanatarajiwa kuukosa mchezo wa kombe la shirikisho hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba sc mchezo utakayofanyika mkoani Songea.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ila watawakosa wachezaji wawili ambao wanasumbuliwa na majeraha.

“Yahya Zaydi na Ally Niyonzima hawa wamebaki Dar kwa kuwa wanasumbuliwa na majeruhi hivyo hawatakuwa kwenye kikosi chetu dhidi ya Simba.

banner

“Kuhusu maandalizi yetu tupo tayari na kila mmoja anahitaji kupata matokeo chanya hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi na kwa namna abavyo wametupokea wanastahili shukrani,” amesema.

Mchezo huo mkali na kusisimua unasubiriwa na wadau wengi wa soka huku mshindi akitarajiwa kukutana fainali ambapo atakutana na mshindi kati ya Yanga sc dhidi ya Biashara United.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited