Home Soka Messi Aweka Rekodi,Barca Akiifunga Mallorca

Messi Aweka Rekodi,Barca Akiifunga Mallorca

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Barcelona wameifunga Real Mallorca mabao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa katika uwanja wa Mallorca jana nchini Hispania.

Artulo Vidal alifunga bao la kwanza baada ya sekunde 66 za mchezo huku Martin Braithwaite akifunga la kwanza kwake na la pili katika mchezo huo kabla ya Jordi Alba kufunga bao la tatu huku Luis Suarez akiingia katika mchezo kwa mara ya kwanza tangu Januari.

Lionel Messi alifunga bao la nne la mchezo likiwa goli la ishirini kwake kwa msimu huu na kuweka rekodi ya kufunga mabao zaidi ya 20 kwa misimu 12 mfululizo.

banner

Ushindi huo umeifanya Barca kuongoza ligi kwa jumla ya pointi 5 huku mpinzani wake mkuu klabu ya Real Madrid wakikabiliana na Elber siku ya jumapili kupunguza gepu la pointi.
–

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited