Home Soka Molinga Bado Kidogo Tu

Molinga Bado Kidogo Tu

by Sports Leo
0 comments

Straika David Molinga amebakiza kidogo kuanza kuichezea timu hiyo katika michuano ya kimataifa baada ya leseni yake kuwa katika hatua za mwisho kukamilika kufuatia kuchelewa kuipata baada ya usajili wake kufanyika mwishoni na kusababisha kuchelewa kutumwa kwa jina lake kwenda shirikisho la soka Afrika(caf).

Molinga na Mustapha Selemani ni wachezaji pekee ambao hawajapata leseni hizo na kushindwa kuichezea timu hiyo katika michuano ya kimataifa.

Uongozi wa Yanga SC, kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Dismas Ten umesema unaendelea kuwasiliana na Shirikisho la Soka barani Afrika CAF, juu ya kupata leseni ya mashindano ya kimataifa kwa wachezaji wao, David Molinga na Mustapha Seleman, ili watumike kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Pyramids FC ya Misri.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited