Home Soka Mtibwa,Yanga Sare

Mtibwa,Yanga Sare

by Dennis Msotwa
0 comments

Timu ya Mtibwa Sugar imeshindwa kuibuka na ushindi katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro baada ya kulazimishwa sare na klabu ya Yanga sc.

Makosa yabeki Said Juma Makapu yaliyompa nafasi Hassani Kihimbwa ambaye alitoa pasi kwa Haruna Chanongo aliyefanikiwa kuandika bao dakika ya 28 bao lililodumu mpaka dakika ya 83 baada ya kusawazishwa na Adeyum Salehe kwa njia ya faulo iliyomshinda kipa Said Nduda na kujaa wavuni.

Mtibwa wanahitaji kushinda mchezo ujao kujihakikishia kubaki ligi kuu baada ya kufikisha pointi 42 huku Yanga wakiwa na pointi 69 nafasi ya pili huku kila timu ikibakiza mchezo mmoja.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited