Kwa mujibu wa bosi anayeshughulikia masuala ya usajili ndani ya klabu ya Yanga Eng.Hersi Said bado siku kadhaa tu watamtambulisha beki kisiki kutoka klabu ya Coastal Union Bakari Nondo Mwamnyeto katika klabu hiyo yenye makao makuu Jangwani Kariakoo.
Bosi huyo wa Gsm kampuni inayojitolea kuihamisha Yanga kwenda mfumo wa mabadiliko alisema hayo leo wakati akifanya mahojiano na kitua cha Wasafi Fm ambapo aliulizwa swali na mwandishi na ndipo alipofunguka kuhusu suala hilo.
“Nikuhakikishie hatujawahi kushindwa lakini kwa sasa Mwamnyeto sio mchezaji wa Yanga wala Simba ila kuna siku utamtambulisha hapa”.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Klabu hiyo imekua ikihusihwa na usajili wa beki huyo aliyejihakikishia namba katika klabu yake mpaka timu ya Taifa ya Tanzania.