Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai amewatembelea wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania(Taifa stars) katika hotel yao waliyoweka kambi nchini Misri Kujiandaa na Michuano ya mataifa ya Afrika (Afcon 2019).
Kiongozi huyo wa chombo kikuu cha kutunga sheria nchini alitembelea kambi hiyo na kuonana na wachezaji na viongozi wa timu hiyo akiwemo kocha mkuu Emmanuel Amunike.
Tanzania imefanikiwa kufuzu michuano hiyo mikubwa barani afrika baada ya miaka 39 kupita tangu washiriki kwa mara ya mwisho.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.