Home Soka Neymar Aiota Barcelona

Neymar Aiota Barcelona

by Sports Leo
0 comments

Neymar yuko tayari kukubali kupunguza asilimia ya mshahara wake kwa asilimia 50′ ili aondoke majira ya joto kutoka Paris Saint-Germain kurudi Barcelona… Nyota huyo wa Brazil amekuwa akihusishwa mara kwa mara na kurudi Camp Nou ingawa bei wanayotaja PSG ilikuwa kubwa na kikwazo kwa Barça kumnasa.

Lakini Imeripotiwa kwamba Neymar ameazimia kulazimisha kurudi kwake Catalonia na atapunguza malipo yake… Neymar anapata £600,000-kwa wiki chini ya mkataba wake wa sasa huko PSG lakini, kwa mujibu wa ripoti hiyo, yuko tayari kupunguza hii hadi £300,000 kwa wiki huko Barcelona.

Hivi Karibuni Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye alitua kwa gharama ya rekodi ya dunia ya pauni 198m wakati PSG ikimsajili kutoka Barcelona mnamo 2017, alikataa mkataba mpya wenye thamani ya Pauni 90m kubakia viunga hivyo vya Parc des Princes… Mkataba wake uliopo sasa unaendelea hadi 2022 na ofa hiyo mpya ingemfunga kwa PSG hadi 2025 lakini Neymar anaonekana kutaka kurejea Barcelona.

banner

cc:Ze chicharito

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited