Home Soka Ni Usiku wa Kisasi Epl

Ni Usiku wa Kisasi Epl

by Dennis Msotwa
0 comments

Timu ya manchester united inatarajiwa kuvaana na Wolverhampton Wonders katika mechi ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza ikiwa ni mchezo wa raundi ya pili wa ligi hiyo yenye wafuasi wengi duniani.

Mechi hiyo itakayopigwa saa nne usiku kwa saa za Tanzania inatarajiwa kuwa mechi ya kulipiza kisasi kwa United baada ya msimu uliopita kufungwa mara mbili na Wolves huku wakitolewa katika kombe la FA  baada ya kufungwa mabao mawili mwezi Aprili mwaka huu.

United haijapata ushindi mbele ya Wolves tangu mwaka 2012 waliposhinda mabao 5-0 katika mechi ya ligi kuu ugenini.

banner

Wolves imeshinda jumla ya mechi 31 kati ya michezi 84 waliyokutana na United huku mashetani wekundu wakishinda mechi 39 huku mechi 14 zikiwa sare.

United wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa na matumaini baada ya kuwafunga Chelsea mabao 4-0 katika mechi ya kwanza huku Wolves wakitoa suluhu ugenini dhidi ya Leicester city.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited