Hatimaye kiungo wa zamani wa Yanga sc na Simba sc Haruna Niyonzima amerudi nyumbani baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na klabu ya As Kigali ya nchini Rwanda.
Kiungo huyo mzaliwa wa Gisenyi nchini humo aliondoka nchini humo miaka kadhaa iliyopita na kuja nchini kujiunga na Yanga sc ambapo alijijengea ufalme baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa zaidi ya misimu mitano na kuamua kujiunga na wapinzani wao Simba sc alipokaa kwa miaka miwili tu.
Awali taarifa zilidai baada ya Simba sc kutoonesha nia ya kumuongezea mkataba kiungo huyo alitakiwa na klabu ya As Vita ya kongo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
As kigali ni timu inayoshiriki ligi kuu nchini Rwanda na itashiriki michuano ya kombe la shirikisho mwakani.