Home Soka Pacome Awasili Kuwawahi Mamelod Sundowns

Pacome Awasili Kuwawahi Mamelod Sundowns

by Sports Leo
0 comments

Staa wa klabu ya Yanga sc Pacome Zouzoua amewasili nchini usiku wa jana kuja kuungana na timu yake kuwahi maandalizi ya mwisho ya mchezo wa hatua ya robo fainali baina ya klabu hiyo na timu ya Mamelod Sundowns utakaofanyika siku ya jumamosi saa tatu usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Staa huyo aliondoka nchini baada ya kuitwa kujiunga na timu ya Taifa ya Ivory Coast kuchukua nafasi ya Ibrahim Sangare, anayeitumikia Klabu ya Nottingham Forest ya Uingereza baada ya mchezaji huyo kupata majeraha siku chache kabla ya kuripoti kambini.

banner

Timu hiyo ya Taifa ilikua na michezo ya kirafiki dhidi ya Benin mnamo Machi 23, 2024 huko Amiens (Ufaransa) na Ivory Coast -Uruguay mnamo Machi 26, 2024 huko Lens (Ufaransa) ambapo staa huyo alikua benchi katika michezo yote miwili ambapo timu yake ilitoa sare ya 2-2 dhidi ya Benin na ushindi wa 2-1 dhidi ya Uruguay.

Staa tayari amewasili nchini mapema usiku wa kuamkia leo na kupokelewa na marafiki zake Yao Kouasi na Aubin Kramo na kuelekea nyumbani ambapo leo atashiriki mazoezi na timu hiyo kambini Avic kujiandaa na mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani wa aina yake.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited