Table of Contents
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera ameahidi kitita cha shilingi milioni 100 kwa wachezaji wa timu hiyo endapo watafanikiwa kuitoa Pyramids fc na kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho.
Zahera ametoa ahadi hiyo baada ya mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika katika uwanja wa nyamgani jijini Mwanza.
Zahera amesema pesa hiyo ameitoa kama motisha kwa wachezaji wake kuhakikisha wanakua na morali ya juu kufanikisha ushindi huo huku akiahidi safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kufanya makubwa siku ya mchezo huo.
Yanga inatarajia kushuka dimbani dhidi ya matajiri hao wa Misri Jumapili hii, baada ya kuondolewa na Zesco United katika hatua ya pili ya Klabu Bingwa Afrika, huku Pyramids wenyewe wakifanikiwa kuiondoa CR Belouzdad ya Algeria kwa uwiano wa mabao 2-1.