Katika kukiimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara na michuano ya kimataifa timu ya Simba sc imemsaini mchezaji mwengine kutoka nchini Brazil na kufikisha idadi ya wachezaji watatu kutoka nchini humo.
Mchezaji huyo anayecheza nafasi ya ulinzi anaitwa Tairone Santos Da Silva mwenye miaka 30 amesaini mkataba wa miaka miwili akitokea nchini brazil katika timu ya Atletico Cearense Fc iliyoanzishwa mwaka 1982 katika mji wa Ceara nchini humo.
Beki huyo mrefu amesajiliwa ili kuziba mapengo ya baadhi ya wachezaji akiwemo Paschal Wawa ambaye amemaliza mkataba na klabu hiyo yenye makao makuu msimbazi jijini Dar es salaam.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.