Wekundu wa Msimbazi Simba SC imetwaa ubingwa wa ligi kuu soka ya Tanzania bara kwa mara ya tatu mfululizo kufuatia Suluhu dhidi ya wenyeji wao Tanzania Prisons mchezo uliochezwa muda mfupi uliopita katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.
Simba imefikisha alama 79 ambazo haziwezi kufikia na timu yoyote ya VPL ikiwa na mechi sita mkononi huku wapinzani wake wanaofuata kwa karibu Yanga na Azam “kama” watashinda mechi zao zote zilizosalia watafikisha alama 78 na 77.
Ni ubingwa wa 21 kwa Simba huku ikiwa nyuma ya mabingwa wa kihistoria nchini Yanga SC iliyotwaa taji hilo mara 27.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.